Posts

Tazama video mpya: Kitu gani - Christina Shusho (Remix)

Image
Hello! Kwa niaba ya team nzima ya Calvary Media, Tunayo-furaha kukusogezea video mpya kabisa toka kwa mkali wa muziki wa injili nchini, Mwanadada  Christina Shusho , wimbo unaitwa  Kitu gani  ni remix ya wimbo wake mwenyewe aliouachia miaka kadhaa iliopita.

Rose Muhando Atiwa Mbaroni mkoani Singida kwa Utapeli

Image
Jeshi  la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za injili, Rose Muhando akituhumiwa kujipati fedha kwa njia ya udanganyifu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Debora Mgiligimba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mwimbaji huyo alikamatwa juzi Wilaya ya Ikungi baada ya wadeni wake ambao ni Waumini wa Kanisa la AICT Singida kupata taarifa kuwa yupo wilayani humo. Inadaiwa kuwa Novemba 3 mwaka jana, mwimbaji huyo alitumiwa fedha na Mwenyekiti wa Kwaya ya Kanisa la AICT Singida, Mashala Japhet Tsh 800,000 ambapo zilitumwa baada ya pande mbili kukubaliana kuwa angekwenda kwenye uzinduzi wa Album ya kwaya na kanisa hilo, hata hivyo hakutokea. Kwa mujibu wa kamanda huyo, uzinduzi wa kwaya hiyo ulikuwa ufanyike Novemba 13 mwaka jana, saa 8 mchana katika uwanja wa Namfua Singida. Novemba 8 mwaka jana, mwimbaji huyo aliomba kutumiwa tena 150,000 kwa ajili ya nauli ya kutoka Dodoma kwenda Sing...

Askofu Gwajima ajibu, baada ya Makonda kumtaja kwenye list ya wahusika wa madawa ya kulevya. (+Video)

Image
Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Bw. Paul Makonda  kutaja kwa kutangaza katika vyombo vya habari  majina 65  ya watu wanaohusika na madawa ya kulevya hapa Tanzania, akiwemo  Manji  ambaye ni mwenyekiti wa club ya yangu,  Mh. Mbowe, Askofu Gwajima  na wengine pia. (Siku ya Jana) Na kuwataka watu wote 65 waliotajwa, kuhakikisha wanaripoti kwenye Kituo Kikuu cha Polisi  Dar es Salaam  (Sentro) siku ya Ijumaa saa 5 asubuhi kwa mahojiano zaidi.  Leo mchana Askofu wa kanisa la Ufufuo na uzima  Mh. Dkt. Gwajima  alikutana na waandishi wa habari na kujibu tuhuma hizo za kuhusishwa na kutajwa kwa kutangazwa kwenye vyombo vya habari kwamba ni muhusika wa madawa ya kulevya na anatakiwa kuripoti sentro polisi Ijumaa saa 5 asubuhi. Bofya Play kutazama majibu  ya Askofu Gwajima kwa makonda.

WIMBO MPYA: MAVUNO - CHRISTINA SHUSHO & MIREILLE BASIRWA.

Image
Mkali wa muziki wa injili hapa Tanzania, mwanadada  Christina Shusho  amekuletea video Mpya inaitwa " MAVUNO ", akishirikiana na  Mireille Basirwa ,

WIMBO MPYA: MONICA - MASANJA MKANDAMIZAJI FT WALTER CHILAMBO.

Image
Download wimbo mpya unaokwenda kwa jina  MONICA  toka kwa  Masanja Mkandamizaji  akiwa  Walter Chilambo . Enjoy!

WIMBO MPYA: HUYU YESU - ANGEL BENARD & MERCY MASIKA.

Image
Leo tumepeata fursa tena ya kukusogezea wimbo mpya  Huyu Yesu  kutoka kwa muimbaji mahiri nchini, mwanadada  Angel Bernad  akiwa na muimbaji mahiri kutoka nchini  Kenya anayefahamika kwa jina la  Mercy Masika  wimbo ukiwa umetengenezwa ndani ya studio ya  Still Alive  iliyopo nchini Kenya.

DOWNLOAD WIMBO MPYA: WALIFIKIRI - MARTHA BARAKA.

Image
Tumekusogezea wimbo mpya  Walifikiri  toka kwa mwanadada  Martha Baraka,  pata fursa ya kudownload hapa.