Posts

BABA KULOLA NATAMANI UNGEKUWEPO UYAONE YANAYOENDELEA KWA ULIOWAACHA.

Image
Aliyekuwa Askofu mkuu wa EAGT Dr. Moses Kulola (Marehemu) Ni miaka mitano sasa tangu aliyekuwa askofu mkuu wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Dr. Moses Kulola afariki dunia August 29,2013 huku kanisa hilo kwa sasa likipita katika mgogoro mkubwa ulioibuka baada ya kile kinachodaiwa kubadilishwa kwa katiba ya kanisa hilo kupitia kikao cha dharura na ubadhirifu wa mali za kanisa unaofanywa na baadhi ya viongozi wajuu wa kanisa. Miongoni mwa vipengele vinavyopingwa na baadhi ya wachungaji wa kanisa la EAGT katika katiba hiyo ni kile kinachoweka ukomo wa uongozi ambapo katiba hiyo inazuia viongozi wa kanisa hilo kuwa na umri unaozidi miaka 70. Mambo mengi yaliibuka huko nyuma ikiwemo kusimamishwa kwa aliyekuwa Askofu mkuu msaidizi  Dr. Mahene mnamo september 17,2016  alisimamishwa uongozi katika maamuzi yaliyofikiwa na baadhi ya viongozi wa dhehebu la EAGT ambao ni Askofu Mkuu, Katibu Mkuu, Mtunza Hazina na Mshauri wa Kanisa kutokana na tuhuma za mmoja wa wat

SIFA JOHN AUKUMBUKA MUZIKI

Image
Mwimbaji wa muziki wa injili Sifa John ambaye alikuwa akifanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa injili miaka kadhaa iliyopita kupitia wimbo wake wa Wateule Tutakwenda ameamua kuweka mtandaoni video za nyimbo zake mbili, Usiku wa kuamkia leo kupitia youtube akaunti yake Sifa John ameweza kupublish video za nyimbo zake mbili ambazo ni Usililie Moyoni na Bwana Ni Mwema, Sifa John amesema amekuwa kimya kwenye muziki kwa muda mrefu ni kutokana na majukumu aliyonayo ya usimamizi wa kituo chake cha watoto yatima kiitwacho Sifa Foundation na kujikuta huku anapotea kabisa, Mwisho Sifa John amewataka mashabiki na wadau wake wasichoke kumvumilia muda si mrefu atarudi kwenye nafasi yake, TAZAMA VIDEO YA SIFA JOHN - USILILIE MOYONI TAZAMA VIDEO YA SIFA JOHN - BWANA NI MWEMA

Download wimbo mpya: Siteketei - Angel Benard

Image
Hello! Leo tumekusogezea wimbo mpya kabisa kutoka kwa Mwanadada  Angel Benard , wimbo unaitwa  Siteketei. 

List ya Wachungaji Matajiri zaidi Duniani 2017 hii hapa.

Image
Zipo list kibao za viongozi wa dini ambazo huonesha namna gani wanakuwa na ushawishi wa kuponya watu kiroho lakini fahamu pia kuwa zipo list za viongozi hao hao wa dini ambao wanatajwa kuwa na fedha nyingi zaidi duniani…na kwa mwaka huu wa 2017 tayari ninayo list ya wachungaji 10 wanaotajwa kuwa na fedha nyingi zaidi duniani.  10. Joseph Prince. Dola Milioni 5  Ni Mchungaji kutoka  Singapore  ambaye anatajwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani  Milioni 5 . Mchungaji  Joseph  hufanya ibada ambazo pia hurushwa LIVE kwenye mtandao wa youtube hivyo kupata umaarufu mkubwa sana barani Asia na duniani.   9. T.B Joshua. Dola Milioni 10  Ni mzaliwa wa  Nigeria  na anatajwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani Milioni 10 . Kwa Nigeria, mchungaji huyu ni maarufu kama Nabii na ana watu wanaomfuatilia kwenye mtandao wa Facebook zaidi ya Milioni 1.5. 8. Billy Graham  Dola Milioni 25  Huyu ni mchungaji wa Marekani na moja kati ya wachungaji wenye umri mkubwa. Alizaliwa mwaka  1918  na k

Kijana wa Miaka 18 Asimulia Jinsi Alivyowateka Watoto Wanne Arusha

Image
Matukio ya utekaji watoto mjini Arusha yameanza kupata mwelekeo wa ufumbuzi baada ya kijana wa miaka 18 kukiri kuwateka watoto wanne alipokamatwa katika mji wa Katoro wilayani Geita alikofanya tukio jingine la utekaji. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari akiwa chini ya ulinzi wa polisi jana, kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Samson Petro alisema watoto wawili aliwarudisha kwa wazazi wao baada ya kupewa Sh300,000. Alisema wengine wawili aliwatelekeza mtaani baada ya wazazi wao kutotoa kiasi cha fedha walichotakiwa kumpa. Samson alisema alianza ‘shughuli’ hiyo ya utekaji watoto kutokana na mahitaji ya fedha na kwamba, aliacha shule akiwa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Lutozo iliyopo Katoro. “Naishi na wazazi wangu, lakini nao ni masikini, nilifanya hivi ili nipate fedha na nilikuwa nikimchukua mtoto naandika ujumbe kwenye karatasi, naandika na namba ya simu napeleka karibu na familia ili wanitafute,” alisema Samson. Awali, kamanda wa polisi

HISTORIA YAVUNJWA AFRIKA YA KUSINI

Image
Dkt Tumishang Makweya Kwa mara ya kwanza katika historia ya muziki wa injili nchini Afrika ya kusini kulishuhudiwa historia kuvunjwa kwa mwimbaji wa muziki wa injili Dr Tumishang Makweya  kuweza kuujaza ukumbi mkubwa kabisa wa burudani uitwayo Dome uliopo jijini Johannesburg usiku wa kuamkia jumatatu Dr Tumi ambaye historia yake ya muziki imeanzia mwaka 2007 akiwa na kundi la Intense, aliweza kuujaza ukumbi huo kwa mara ya kwanza baada ya kushuhudia tukio kama hilo kwa mwimbaji wa muziki wa dunia Casper Nyovest ambaye aliujaza ukumbi huo october mwaka 2015 na kuacha historia nchini humo hadi kupongezwa na Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma. The Dome, ukumbi mkubwa Johannesburg Ukumbi huo wenye uwezo wa kuingiza watu 19,000 waliokaa na zaidi ya 2000 waliosimama, hufanyika maonyesho ya kimataifa ya biashara kutokana na ukubwa wake na hata kwa upande wa muziki watu wenye uwezo wa kuujaza ukumbi huo ni waimbaji wa kimataifa au kundi kubwa kama Joyous ambao hata hivyo hawajawahi ku

Download wimbo: Umenifanya ibada - Paul Clement.

Image
Leo tumepata fursa ya kukusogezea wimbo huu  Umenifanya Ibada  toka kwa Paul  Clement . Ni moja kati ya nyimbo ambazo zimekonga sana mioyo ya wasikilizaji ndani na nje ya nchi.