BABA KULOLA NATAMANI UNGEKUWEPO UYAONE YANAYOENDELEA KWA ULIOWAACHA.


Aliyekuwa Askofu mkuu wa EAGT Dr. Moses Kulola (Marehemu)
Ni miaka mitano sasa tangu aliyekuwa askofu mkuu wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Dr. Moses Kulola afariki dunia August 29,2013 huku kanisa hilo kwa sasa likipita katika mgogoro mkubwa ulioibuka baada ya kile kinachodaiwa kubadilishwa kwa katiba ya kanisa hilo kupitia kikao cha dharura na ubadhirifu wa mali za kanisa unaofanywa na baadhi ya viongozi wajuu wa kanisa.
Miongoni mwa vipengele vinavyopingwa na baadhi ya wachungaji wa kanisa la EAGT katika katiba hiyo ni kile kinachoweka ukomo wa uongozi ambapo katiba hiyo inazuia viongozi wa kanisa hilo kuwa na umri unaozidi miaka 70.

Mambo mengi yaliibuka huko nyuma ikiwemo kusimamishwa kwa aliyekuwa Askofu mkuu msaidizi  Dr. Mahene mnamo september 17,2016 alisimamishwa uongozi katika maamuzi yaliyofikiwa na baadhi ya viongozi wa dhehebu la EAGT ambao ni Askofu Mkuu, Katibu Mkuu, Mtunza Hazina na Mshauri wa Kanisa kutokana na tuhuma za mmoja wa watumishi ya makanisa ya EAGT kwamba ameota ndoto kuwa kiongozi huyo amezaa nje ya ndoa yake jambo ambalo ni kinyume na maadili ya uongozi wa dhehebu hilo.

Mpaka sasa kanisa hilo halijafikia muafaka na kesi bado ipo mahakamani.


Comments

Popular posts from this blog

YAJUE MAKANISA MAKUBWA ZAIDI DUNIANI