T.B Joshua Azua Gumzo Baada Ya Kununua Ndege Yake Binafsi.


Mchungaji na kiongozi wa makanisa ya ‘Synagogue Church of All Nation’ TB Joshua

Mchungaji na kiongozi wa makanisa ya ‘Synagogue Church of All Nation’ TB Joshua, ameingia kwenye ‘list’ ya wachungaji wachache wanaomiliki ndege binafsi barani Afrika.
Joshua, mwenye maskani yake nchini Nigeria, ametoa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 60 ili kumiliki ndege hiyo aina ya Gulfstream G550.
Kwa mujibu wa kituo cha Habari cha Sahara, stakabadhi ya ununuzi wa ndege hiyo ulifanyika tangu Aprili mwaka huu.
Taarifa za ndani zaidi zinadai TB Joshua, mwanzoni aliletewa ndege hiyo Disemba mwaka 2013 kwa ajili ya kuiona ili akiridhika nayo utaratibu wa manunuzi ufatwe.
Hata hivyo serikali ya Nigeria, imepanga kufanya uchunguzi kubaini mapato kamili ya kanisa la mchungaji huyo.


Comments

Popular posts from this blog

YAJUE MAKANISA MAKUBWA ZAIDI DUNIANI