T.B Joshua Azua Gumzo Baada Ya Kununua Ndege Yake Binafsi.

Mchungaji
na kiongozi wa makanisa ya ‘Synagogue Church of All Nation’ TB Joshua, ameingia
kwenye ‘list’ ya wachungaji wachache wanaomiliki ndege binafsi barani Afrika.
Joshua,
mwenye maskani yake nchini Nigeria, ametoa kiasi cha dola za Kimarekani milioni
60 ili kumiliki ndege hiyo aina ya Gulfstream G550.
Kwa
mujibu wa kituo cha Habari cha Sahara, stakabadhi ya ununuzi wa ndege hiyo
ulifanyika tangu Aprili mwaka huu.
Taarifa
za ndani zaidi zinadai TB Joshua, mwanzoni aliletewa ndege hiyo
Disemba mwaka 2013 kwa ajili ya kuiona ili akiridhika nayo utaratibu wa
manunuzi ufatwe.
Hata
hivyo serikali ya Nigeria, imepanga kufanya uchunguzi kubaini mapato kamili ya
kanisa la mchungaji huyo.
Comments
Post a Comment