WASANII WA GOSPEL KUTOA WIMBO MAALUM KUHAMASISHA AMANI.

images

WAIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili wanatarajiwa kutoa wimbo maalum wa kuhamasiaha amani na upendo wakati wa Tamasha la Amani Oktoba 4 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa amezungumza na waimbaji hao na wamekubaliana watatunga wimbo maalum watakaouimba kwa pamoja siku hiyo.

Alisema wimbo huo utaitwa Amani na Upendo na kwamba maandalizi yanaendelea kuhakikisha wasanii wengi maarufu wanakuwepo.

 “Watakuwa wasanii maarufu, naamini wengi waliokuwepo kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu watashiriki katika wimbo huo.

“Tunaandelea na mazungumzo na wasanii mbalimbali, ambapo tayari Rose Muhando ameshakubali kutumbuiza na wengine tuliowatangaza,” alisema Msama.

Baadhi ya wasanii maarufu ambao wamewahi kushiriki matamasha yanayoandaliwa na Msama ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.
Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Sohly Mahlangu.

Comments

Popular posts from this blog

YAJUE MAKANISA MAKUBWA ZAIDI DUNIANI