MHE. PAUL MAKONDA AMSHUKURU MUNGU KUMUWEZESHA KAZINI.


                                   Mh. Paul Makonda akiwa na Mke wake akimshukuru Mungu.

Mheshimiwa Paul Makonda Jumapili alikuwa anatimiza mwaka mmoja tangu kuteuliwa kwake kuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Jumapili iliyopita katika ibaada kanisani Living water center ministry Kawe alipolelewa kiroho na anapoabudu alienda kumshukuru Mungu na kutoa sadaka ya shukrani kwa hatua aliyoifikia.
Katika ibaada hiyo Mh.Paul Makonda aliongozana na mke wake;alipopewa nafasi ya kuzungumza alisema anamshukuru Mungu kwa kutimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni akisema haikuwa rahisi kwake ila Mungu amemuwezesha,pia aliongeza kusema "usishindwe kufanya mambo ya kimaendeleo kwa changamoto za kimazingira au chochote kama kwangu ambavyo imekuwa ikionekana"


Mapema akimkaribisha kuzungumza Mhe. Paul Makonda Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi alikuwa anaelezea jinsi ambavyo amemlea kiroho Mh.Makonda hata kabla ya kuingia kuwa mtumishi wa serikali jinsi alivyokuwa mbunifu wa shughuli mbalimbali hivyo kinachofanyika leo sio kipya kwake.

Baada ya Ibada hiyo ya shukrani Bwana akatenda zaidi kwa kumfanya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Hongera Paul Makonda kwa kuteuliwa kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam.


                         Mh. Paul Makonda alipokuwa akizungumza



                  Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe Apostle Onesmo Ndegi 


Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre alipokuwa akiwaeleza waumini kuhusu Mh. Paul Makonda


Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre alipokuwa akiwaeleza waumini kuhusu Mh. Paul Makonda.



                                     Mh. Paul Makonda akiwa akifafanua jambo


Maombi yalifanyika kwake na mke wake ili Mungu amtangulie katika utumishi wake serikalini.






Apostle Onesmo Ndegi,Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe akifanya maombi kwa watu waliokuja mbele kuokoka katika ibada hiyo.



                                  maombi kwa watu waliokuja mbele kuokoka katika ibada





Comments

Popular posts from this blog

YAJUE MAKANISA MAKUBWA ZAIDI DUNIANI