MUISLAMU AUWAWA BAADA YA KUWATAKIA HERI YA PASAKA WAKRISTO.
![]() |
Marehemu Asad Shah ©ChristianPost |
Asad Shah mwenye umri wa miaka 40 amekutwa na umauti masaa machache baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa facebook tarehe 24 Machi kuhusiana na sikukuu ya pasaka, ambapo Wakristo duniani huadhimisha kufa na kufufuka kwa BWANA na Mwokozi wao, Yesu Kristo.
![]() |
Mashada kumuenzi Asad. Moja ya picha iliyopo kwenye tovuti ya kumuenzi ©Asad Shah Memorial |
Tofauti na matarajio ya kutafuta pauni 1,500 ambayo ni sawa na takribani shilingi milioni 4 na nusu kwa fedha Tanzania, kiasi kilichochangwa kimezidi kwa zaidi ya mara sabini, na kufikia takribani pauni laki moja na kumi na moja, sawa na zaidi ya shilingi milioni 340; kiasi ambacho kimechangwa na watu elfu 5 hadi hivi hivi sasa.
Picha kutoka tovuti inayokusanya fedha za kusaidia familia ya marehemu ©gofundme |
Hata hivyo pamoja na kuaminika kwamba chanzo cha kifo chake kinatokana na kuwatakia heri wakristo, baadhi ya fununu zinaeleza kwamba Shah amekuwa akipokea vitisho vya aina mbalimbali kutokana na baadhi ya waislamu wenye msimamo mkali kuamini kwamba yeye ni nabii wa uongo.
Kwa mujibu wa kiongozi wa msikiti wa Glasgow Ahmadi, Bwana Owusu Konadu, ameeleza kwamba iwapo Shah angetoa taarifa mapema kwenye uongozi wa msikiti huo basi nao wangelifikisha taarifa hizo polisi ili zipate kufanyiwa kazi, lakini aliamua kuwa kimya.
Taarifa za kutishiwa zimepatikana baada ya rafiki wa marehemu kupitia kurasa zake za kijamii na hivyo kuona kilichokuwa kinaendelea. Hata hivyo bado inaaminika kwamba upendo wake kwa kila mtu ndio umepelekea mauti yake.
Christian Post imeandika
Comments
Post a Comment