MUUZA MADAWA MAARUFU ATAFUTA FARAJA KUPITIA KITABU CHA PURPOSE DRIVEN LIFE.
![]() |
Guzman "El Pacho" akiwa amekamatwa upya Januari 2016 |
Machache haya yaonyeshayo umuhimu wa vitabu, yamefanya mfanyabiashara wa madawa haramu ya kulevya duniani, Joaquin Guzman ambaye anatumikia kifungo cha maisha kwenye jela mojawapo nchini Mexico kuanza kusoma kitabu cha Mchungaji Rick Warren; The Purpose Driven Life.
Kitabu hicho maarufu duniani kinafahamika hasa kwa kutoa hamasa kwa watu kujitambua na kufanya kile wanachostahili, huku ikiwa imesheheni maandiko kadha wa kadha kutoka kwenye Biblia.
Kwa mujibu wa maofisa wa polisi, Guzman maarufu kwa jina la El Chapo, ameanza kusoma kitabu hicho kilicho kwenye tafsiri ya lugha ya spanish, ambapo kwa hivi karibuni baada ya kutoroka jela na kukamatwa tena januari 2016, amenyimwa fursa ya kutazama runinga, huku vitabu akipewa.
Pamoja na hilo, maofisa wameongeza ulinzi maradufu kwenye selo yake, huku walinzi wawili wakimlinda usiku na mchana, pamoja na mbwa mmoja ambaye ana kazi maalumu ya kuhakikisha chakula anachopewa El Chapo hakina sumu ya aina yoyote ile.
"Wakati unazaliwa ulimwenguni, Mungu alikuwapo kama shahidi asiyeonekana, akitabasamu kuhusu ujio wako. Alitaka uwe hai, na ujio wako ulimpa faraja kubwa sana. Mungu hakuhitaji kukutengeneza tu, bali aliamua kukutengeneza ili apat kufurahi."
Ni sehemu ya maneno ya Rick Warren, ambaye anasomwa na adui mkubwa kwenye mapambano ya madawa ya kulevya duniani, akiwa jela kwa sasa.
Associated Press.
Comments
Post a Comment