TEMBONI KKKT YAZINDUA JENGO KUBWA NA LA KISASA LA KANISA.
Askofu mkuu aliyemaliza muda wake, ambaye pia ni askofu mkuu wa Dayosisi ya mashariki na Pwani kanisa la Kiinili la Kilutheri nchini (KKKT) Dkt Alex Gehaz Malasusa hapo jana aliwaongoza mamia ya waumini wa kanisa hilo usharika wa Temboni jijini Dar es salaam katika ufunguzi rasmi wa jengo jipya la ibada ambalo limechukua takribani miaka mitano kuanzia ujenzi hadi kukamilika kwake.
Askofu Malasusa pia alisindikizwa na baadhi ya wachungaji wa Dayosisi hiyo, ambapo ibada hiyo iliyofana pia ilihudhuriwa na ndugu, marafiki na wageni mbalimbali walioalikwa na usharika huo wa Temboni jijini Dae es salaam.Kanisa la Kilutheri nchini limekuwa mstari wa mbele kupitia sharika zake kwa kujenga majengo mazuri ya ibada na ya kisasa ukilinganisha na makanisa mengine ambapo licha ya majengo lakini pia katika suala la Kiroho sharika za kanisa hilo limekuwa likiwaacha midomo wazi baadhi ya waumini wa makanisa mengine kutokana na muamko mkubwa kwenye maombi na maombezi, ibada za kusifu na kuabudu na masuala yote ya kuwaweka watu karibu na Mungu.
![]() |
Waumini wakiwa nje ya jengo lao mara baada ya ibada kukamilika ©JamesSabuni |
Comments
Post a Comment