NYOTA WA MUZIKI WA INJILI KATIKA MAPAMBANO NA MASHABIKI WAKIMKATAZA KUCHORA TATTOO MWILINI
Nyota wa muziki nchini Afrika ya kusini ambaye pia ni mchungaji wa moja ya kanisa nchini humo kijana Khaya Mthethwa ambaye alikuwa mshindi wa shindano la SA Idol mwaka juzi pia amewahi kuwa mwimbaji wa Joyous Celebration, amejikuta katika mapambano na mashabiki pamoja na rafiki zake katika Facebook baada ya mwimbaji huyo alipoandika kwamba anataka kujichora tattoo na kuacha swali kwamba ndio au hapana, ambapo alipata upinzani mkali wakipinga asijichore tattoo
Khaya ambaye alikuwa matembezini jijini New York nchini Marekani kwa takribani wiki tatu, aliweza kuwajibu na kuwauliza maswali watu hao ambao wengine walidai kujichora ni dhambi kama Mungu aliona inapendeza basi angewafanya magazeti ili wajichore lakini haikuwa hivyo, kitendo ambacho pia mwimbaji huyo anayetamba na DVD yake mpya ya The Uprising New Dawn kuwauliza kama ni hivyo kwanini nawao wadada wanavaa hereni na mapambo mengine kwakuwa yeye pia anajua kwamba kujichora ni mojawapo ya kutunza mwili wake kwa utukufu wa Mungu
Comments
Post a Comment