Mtokambali:Taifa bila maono haliwezi kuendelea katika Nyanja za uchumi.


Kiongozi wa madhehebu ya TAG nchini amesema, taifa lolote haliwezi kuendelea kama viongozi wake hawana maono ambayo yataleta mabadiliko ya kimaendeleo katika nyanja zote zikiwemo za kiuchumi, elimu, afya na miundombinu ya barabara kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wake.

Kiongozi huyo makamu wa rais wa makanisa ya TAG kanda ya AFRIKA, ambaye pia ni askofu mkuu wa kanisa hilo hapa nchini, askofu Dkt. Barnabas Mtokambali katika ibada ya uzinduzi wa jimbo la Tabora kasikazini na kusimikwa kwa askofu mpya wa jimbo hilo ambapo amesema, mafanikio ya serikali ya awamu ya tano yanatokana na maono ya mbali ya rais Dkt, John Pombe Magufuli.

Aidha mgeni rasmi katika ibada hiyo mkuu wa wilaya ya Nzega, akitoa rai kwa viongozi wa madhehebu ya dini amesema kuwa wilaya ya Nzega inakabiliwa na changamoto ya mauaji ya ya kikatili hivyo ni fursa kwa viongozi kujikita vijijini ambapo inaonyesha imani za dini bado ni duni.
Kwa upande wake askofu mteule wa jimbo hilo, Mhashamu Endrew Kayamba amesema kuwa, jukumu kubwa la kanisa ni kuwafikia watu wengi vijijini ambapo kuna uelewa duni wa kumjua Mungu na kuthaminiana jambo ambalo husababisha uasi.

Comments

Popular posts from this blog

YAJUE MAKANISA MAKUBWA ZAIDI DUNIANI