HISTORIA YAVUNJWA AFRIKA YA KUSINI

Dkt Tumishang Makweya

Kwa mara ya kwanza katika historia ya muziki wa injili nchini Afrika ya kusini kulishuhudiwa historia kuvunjwa kwa mwimbaji wa muziki wa injili Dr Tumishang Makweya  kuweza kuujaza ukumbi mkubwa kabisa wa burudani uitwayo Dome uliopo jijini Johannesburg usiku wa kuamkia jumatatu
Dr Tumi ambaye historia yake ya muziki imeanzia mwaka 2007 akiwa na kundi la Intense, aliweza kuujaza ukumbi huo kwa mara ya kwanza baada ya kushuhudia tukio kama hilo kwa mwimbaji wa muziki wa dunia Casper Nyovest ambaye aliujaza ukumbi huo october mwaka 2015 na kuacha historia nchini humo hadi kupongezwa na Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma.
The Dome, ukumbi mkubwa Johannesburg
Ukumbi huo wenye uwezo wa kuingiza watu 19,000 waliokaa na zaidi ya 2000 waliosimama, hufanyika maonyesho ya kimataifa ya biashara kutokana na ukubwa wake na hata kwa upande wa muziki watu wenye uwezo wa kuujaza ukumbi huo ni waimbaji wa kimataifa au kundi kubwa kama Joyous ambao hata hivyo hawajawahi kufanya onyesho katika ukumbi huo.
Baadhi ya waimbaji maarufu waliompongeza kwa hatua hiyo aliyofikia kimataifa katika kuujaza ukumbi huo, ni pamoja na mkurugenzi wa kundi la Joyous Celebration Pastor Jabu Hlongwane, waimbaji waliowahi kuimba kundi hilo na watu wengine maarufu.
Wazo la kufanyia tamasha lake kwenye ukumbi huo alilitoa mapema mwezi May mwaka huu kupitia anuani zake za mitandao ya kijamii akisema “nafikiria kuujaza The Dome kwa ajili ya Yesu” hatua ambayo alitiwa moyo na watu wanaomfatilia kwa karibu.
Dkt Tumi na familia yake
Dr Tumishang Makweya alizaliwa jimbo la Limpopo Afrika ya kusini, alifunga ndoa mwaka 2008 na Kgaugelo na kujaaliwa kupata watoto watatu katika ndoa yao, ni daktari kweli wa binadamu mwenye ofisi yake ya kidaktari. Alianza uimbaji akiwa na kundi la Intense mwaka 2007 kabla ya kuanza kuimba kwa kujitegemea. Baba yake alikuwa mchungaji wakati mama yake alikuwa ni mwalimu. Licha ya kuwa ni mwimbaji mzuri lakini pia anajulikana kwakuwa mwandishi bora wa nyimbo mfano ambao unaweza kuonwa kupitia album yake mpya ya Heart of A King ambayo nyimbo zote 16 zimeandikwa nayeye album ambayo ilitanguliwa na Love and Grace iliyomtambulisha vyema ikiwa imebeba wimbo kama Nothing without you
Dr Tumi na wazazi wake

Comments

Popular posts from this blog

YAJUE MAKANISA MAKUBWA ZAIDI DUNIANI